Ingia / Jisajili

Yesu Kazaliwa

Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Reuben Maghembe

Umepakuliwa mara 1,096 | Umetazamwa mara 2,998

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Tuimbe aleluya Yesu kazaliwa (leo) *2

Twende sote kule Bethlehemu tukamwone (leo)

Mkombozi wetu Yesu leo kazaliwa

Shangwe leo twimbe sote furaha njoni sote twimbe chereko leo Yesu kazaliwa *2

 

BETI

1.       Malaika wa Bwana alipowatokea wale wachungaji akasema msiogope mimi ninawaletea habari njema

2.       Kwa kuwa leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi Yesu yeye ndiye mwenye uweza wa kifalme mabegani mwake

3.       Amezaliwa kama alivyotabiriwa na manabii Kristo Masiha Mkombozi wa ulimwengu ameshuka kutuokoa

4.       Pande zote za dunia zimeuona zimeuona wokovu wake nasi tuimbe kwa furaha twimbe aleluya


Maoni - Toa Maoni

FELIX JUMA Dec 08, 2024
Good song

Toa Maoni yako hapa