Mtunzi: Joseph Makoye
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Makoye
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Michael Nkana
Umepakuliwa mara 3,090 | Umetazamwa mara 6,259
Download Nota Download MidiKiitikio
//:Yesu Kristo kweli kafufuka(kafufuka) minyororo ya shetani kaivunja://
//: Uwinguni waimba Aleluya dunia twaimba aleluya sote tuna mshangilia mwana wa maria://
Mashairi
1. Wafurahi leo watakatifu wote, wafurahi leo malaika wa mbinguni, tufurahi pia na sisi binadamu tuimbe aleluya
2. Mwimbie ni Bwana kwa shangwe na furaha, na vigeregere visikike duniani, msifuni Bwana kwa nyimbo na zaburi, ni kweli kafufuka.
3. Enezeni kote habari njema hii, tangazeni pote maajabu yake Bwana, Kristo alikufa na leo kafufuka, hili ni fumbo kubwa.