Ingia / Jisajili

Yesu Ni Mwangaza

Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Derick Wafula

Umepakuliwa mara 1,808 | Umetazamwa mara 5,330

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Ndipo ukatema mate, aridhini, ukalifanya tope, mkononi
Ukampaka kipofu , ma-choni, macho yakafunguka, akaona, 
Na mimi ni kipofu, nifumbue, macho ya roho yangu, kwa maana
{
{/ s/ Mwangaza ni wewe, Mwokozi ni wewe
Mwalimu ni wewe, Kiongozi ni wewe 
/ w / Ni wewe mwangaza na ni wewe Mwokozi
Ni wewe mwalimu na ni wewe kiongozi </b>} *2 Yesu
} *2

2. Ukamshusha kutoka,  kwenye mti, Yule mtu mfupi, wa ushuru
Ukala nyumbani mwake, Zakayo, na ukamfundisha, kugeuka
Naye akakusikia, mwalimu, kageuza mwenendo, kwa maana

3. Naomba niongoze, ee Yesu, nibadili mwenendo, nigeuke
Njia inipotoshayo, niiache, uniponye usugu, wa moyoni
Dhambi niirudiayo, niishinde, nifundishe niweze, kwa maana

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa