Ingia / Jisajili

Aleluya Tumshukuru Mungu

Mtunzi: Augustine Rutakolezibwa
> Mfahamu Zaidi Augustine Rutakolezibwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Augustine Rutakolezibwa

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: AUGUSTINE RUTAKOLZIBWA

Umepakuliwa mara 1,285 | Umetazamwa mara 4,088

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Aleluya twimbe aleluya
Tumshangilie Mungu mkuu pia tumshukuru
Ametuumba akatuweka mpaka hii leo tushukuru
Yeye hutoa majira ya mwaka, masika na kiangazi tuvitumie kwa maendeleo twashukuru
Mvua inanyesha, tunapata chakula, twashukuru Mungu mkuu tunashukuru Mungu ahsante
Wanyama na ndege uliowaumba wawapa chakula cha kutosha
Hawapandi hawavuni wewe huwalisha
Uifiwe Mungu mkuu kwa ulivyoviumba
Jua, mwezi, nyota, anga, vyatangaza ukuu wa Mungu
Atukuzwe Mungu Baba, Mwana na Mungu Roho, wote ni Mungu mmoja
Njoni tumshukuru Mungu wetu
Tumshukuru kwa pumzi ya uhai
Toka kuzaliwa mpaka hii leo, Baba tunakushukuru
Tunashukuru Baba ahsante kwa mema yako
Tnashukuru kwa kutujalia baraa na nguvu kila siku
TUNAKUSHUKURU

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa