Mtunzi: Joseph C. Shomaly
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph C. Shomaly
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo | Mwanzo | Shukrani
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 25,570 | Umetazamwa mara 38,070
Download Nota Download MidiAlfajiri ya Kupendeza
Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka
Jua limekwishachomoza, laamsha wote waliolala
Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba
(Njooni)
{Njooni baba mama na watoto
Njoni wote mbele za Bwana
Tumtolee shukrani zetu, kwa kutoa sadaka } *2
1. Ndege wanamshukuru, kwa sauti za kupendeza
Na sisi tumshukuru, kwa zawadi alizotupa (Njooni)
2. Wanyama pia na mimea, vyote vimeumbwa na Mungu
Vitu vyote vya duniani, vyapaswa kumshukuru Mungu
3. Aliumba dunia hii, kaweka giza pia mwanga
Mchana tufanyeni kazi, usiku na tupumzike (Njooni)
Alfajiri ya Kupendeza
Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka
Jua limekwishachomoza, laamsha wote waliolala
Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba
(Njooni) {Njooni baba mama na watoto