Mtunzi: Joseph C. Shomaly
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph C. Shomaly
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 2,153 | Umetazamwa mara 5,947
Download Nota Download Midi1. Hii sio hadithi ninataka kusimulia
Wala sio historia wala si somo la siasa
Ni mambo mema sana aliyotenda Mungu kwangu
Na nisipoyatamka nitakuwa sina fadhila
Wazazi wamenilea mpaka nimefika hapa
Majirani na ndugu zangu pia wamenipiga jeki
[ b ] Baba usikie sala hii mimi natoa
{ Wabariki wazazi wangu wape maisha marefu
Wabariki na ndugu zangu wape amani tele
Marafiki zangu pia mimi mwenyewe
Siwezi kusahau kuwaombea na adui zangu } *2
2. Mungu ninakushukuru, afya njema wanijalia
Kila ninapoamka sijui nitakupa nini
Masomo yangu nasoma pia ninafaulu vyema
Sasa nimefika hapa sio kwamba mimi ni mwema
3. Shuleni niliposoma nilikuwa na marafiki
Waliosoma vizuri pia na wenye afya njema
Sio wote waliweza kufikia nilipofika
Nashindwa niseme nini jinsi umenipenda mimi
4. Vijijini nimeishi watu wengi nimewaona
Hawana mbele na nyuma wameishia kunywa pombe
Maisha yao magumu elimu yao haba haba
Nashindwa nikupe nini hapa nilipofika mimi
5. Siwezi kusema mengi najua wewe ndiwe kinga
Nibariki nijalie maisha yenye kupendeza
Kipaji nilicho nacho cha kuimba na kuhubiri
Kiwavute watu wengi wakuabudu wewe Bwana