Ingia / Jisajili

Alidharauliwa Na Kukataliwa

Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma

Umepakiwa na: Martin Munywoki

Umepakuliwa mara 1,308 | Umetazamwa mara 3,658

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
ALIDHARAULIWA! 
(Is 53)


Alidharauliwa na kukataliwa kukataliwa na watu 
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko 


1. Alikua mbele zake kama mche mwororo, na kama mzizi katika nchi nchi kavu
Hakuwa na umbo kuvutia wala uzuri, hata tumwonapo tumtamani!
Ni kama mtu ambaye watu humficha uso, wala hatukumhe-sabia kuwa kitu
 

2. Hakika amechukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu amejitwika
Lakini na sisi tulidhani kuwa kapigwa, amepigwa na Mungu na kuteswa!
Bali alijeruhi-wa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu maovu yetu


3. Adhabu ya amani yetu ilikuwa kwake, na kwa kupigwa kwake yeye sisi tumepona
Sisi sote kama ko-ndoo tumepotea,  kila mmoja njia yake yeye!
Bwana ameweka juu yake maovu yetu, alionewa lakini alinye-nyekea


4. Alionewa lakini hakufunua kinywa, kama mwanakondoo akipelekwa machinjoni
Kwa kuonewa kuhukumiwa kaondolewa, ni nani atasimulia haya?
Ni nani aliyesa-diki habari hii, na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?
martinmunywoki@gmail.com
+254718801590

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa