Ingia / Jisajili

Shikilia Usiachie

Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Eusebius Joseph Mikongoti

Umepakuliwa mara 421 | Umetazamwa mara 2,144

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1a) Safari uliyoanza mwenzangu, ya kuelekea juu mbinguni, usiachie katikati,

  b) Japo ina vikwazo na machungu, kumbuka ilianza utotoni, shikilia usiachie

Kiitikio

[(Shikilia) ndugu yangu (usiachie) shika sana x2] ulicho nacho usichanyang'anywe.

2a). Talanta uliyopewa e dada, ndugu endelea kuizalisha, usije uka inyang'anywa,

  b).  Na kupewa aletaye faida, tazama siku zinaisha isha, shikilia usiachie.

3a). Bidii uliyo nayo kuomba, maisha yanapo kuwa magumu, usiitelekeze kamwe,

  b). Hata maisha yakiwa sambamba, daima katika sala udumu, shikilia usiachie


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa