Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Eusebius Joseph Mikongoti
Umepakuliwa mara 781 | Umetazamwa mara 3,056
Download Nota Download MidiPENDO LA MARAFIKI
// u t a n g u l i z i //
Ninyi ndinyi mmenikamilisha kamilisha (hadi)
Hadi nikawa hi-vi mi-mi nilivyo (ndugu zangu)
Ni Mungu Baba ndiye aliyetukutanisha (japo)
Japo hatulingani tumekamilishana
{Katika pendo lenu – ndipo nimeelewa jinsi Mungu alivyo
Nimemuona – Mungu macho kwa macho } *2
// k i i t i k i o //
[ s ] Nikiwa na njaa –
Ni ninyi marafiki zangu mnimegeao mkate
[ a ] Penye machungu na maumivu makali –
Ni ninyi marafiki zangu mwaniuguza majeraha
[ t ] Nikitawaliwa na hofu –
Ni ninyi marafiki zangu mnaonipa moyo upya
[ b ] Tena nikipotea njia –
Ni ninyi marafiki zangu mwanirudi mwanikosoa
// m a s h a i r i //
1. Ona tunavyosaidiana hima, wenyewe kwa wenyewe,
Wakati wa furaha hata wa shida
Tumeweka mbali tofauti kidaraja na mali
Bahati iliyoje kuwa pamoja
2. Ona chuki, wivu, fitina, umimi, havimo kati yetu
Wakati wa furaha hata wa shida
Tumeweka msingi imara usiotikisika
Bahati iliyoje kuwa pamoja
// h i t i m i s h o //
{ Pendo pendo pendo pendo –
pendo letu lidumu milele
Tuombeane tusaidianeni –
waone Mungu kati yetu } *2
Wasitenganishwe – wapendanao
Waombeeni - baraka tele
sitenganishwe – wapendanao
Waombeeni - baraka tele, pendo na lidumu