Maneno ya wimbo
ASANTE BABA
1. Umenilisha mwili wako pia damuyo, ukakubali nishiriki karamu yako
Unaujua udhaifu wangu wote, neema yako yaangaza nipitapo ee Baba
Mimi ninakushukuru, asante ee Baba, yote unijaliayo asante ee Baba, ndiwe tegemeo langu
asante ee Baba
Naja na shukrani zangu asante ee Baba, mbele yako ninasema asante ee Baba, leo
ninakushukuru asante ee Baba
2. Kila mara nitokapo hapa narudi mzima, ishara kuwa Mungu wanipenda
3. Kila mara nakuita wewe wanisikiliza, ishara kuwa Mungu wanipenda
4. Kila mara naanguka wewe unaniinua, ishara kuwa Mungu wanipenda
5. Chanzo cha furaha yangu wewe Mungu ni wewe, Mungu wangu ni wewe unipaye nguvu
nikutumikie milele
Ninayemtumikia wewe Mungu ni wewe Mungu wangu ni wewe,nayo nyumba yangu
nakutumikia milele
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu