Mtunzi: Emanuel Chisunga Kasebe
> Mfahamu Zaidi Emanuel Chisunga Kasebe
> Tazama Nyimbo nyingine za Emanuel Chisunga Kasebe
Makundi Nyimbo: Shukrani | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Emanuel Kasebe
Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiKiitikio
Asante baba nashukuru, Asante kwa wema wako, mema mengi wanijalia mazuri siwezi kulipa,
Asante Mimi nitakushukuru (Mungu) Nimekula nimeshiba nimeshiba Asante. X2
1. (a)Niwapo na shida katika Maisha wanifariji,
(a) Nikisafiri sina hofu tena bwana waniongoza,
Asante Mimi ninakushukuru wewe ni ngome na ngao yangu.
2. (a) Nikataliwa na ndugu zangu Wala sina hofu
(b) Tumaini langu lipo kwako bwana hutaniacha,
Asante Mimi ninakushukuru wewe ni ngome na ngao yangu.
3. (a) Mara nyingine nakukosea bwana wanisamehe
(b) Unanionya na kunionesha njia iliyo Bora
Asante Mimi ninakushukuru wewe ni ngome na ngao yangu.