Mtunzi: James Chusi
> Tazama Nyimbo nyingine za James Chusi
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: James Chusi
Umepakuliwa mara 2,549 | Umetazamwa mara 5,486
Download NotaBwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu
Mkono wa kuume wake Mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umetenda wokovu
2. Bwana ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake
3.Miisho yote ya dunia imeuona,
Wokovu wa Mungu wetu,
Mshangilieni Bwana, Nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha.