Mtunzi: Haule Alfonce Innocent
> Tazama Nyimbo nyingine za Haule Alfonce Innocent
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Alfonce Haule
Umepakuliwa mara 2,858 | Umetazamwa mara 5,161
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 16 Mwaka C
Kiitikio: Bwana ni nani, atakaye kaa katika hema yako, ni nani atakayekaa katika hema yako. X 2.
1 (Sauti ya I & II). Bwana ni nani, atakayefanya maskani, maskani yake katika kilima chako, kilima chako kitakatifu?
(Sauti ya III & IV). Ni yeye aendae kwa ukamilifu, na kutenda haki asemaye kweli, asiyesingizia kwa ulimi wake.
2. (Sauti ya I & II). Yeye ambaye, hakumtenda mwenziwe mabaya, wala hakumsengenya jirani yake, machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa!
(Sauti ya III & IV). Bali huwaheshimu wamchao Bwana, hakutoa fedha yake apate, fedha yake apate kula riba.
3. (Sauti ya I & II). Hakutwaa rushwa, amwangimize asiye na hatia,
(Sauti ya III & IV). Mtu atendaye mambo haya (Wote): Hataondoshwa milele.