Ingia / Jisajili

Nchi Imejaa Fadhili Za Bwana

Mtunzi: Haule Alfonce Innocent
> Tazama Nyimbo nyingine za Haule Alfonce Innocent

Makundi Nyimbo: Juma Kuu

Umepakiwa na: Alfonce Haule

Umepakuliwa mara 598 | Umetazamwa mara 1,976

Download Nota
Maneno ya wimbo

Kiitikio: Nchi imejaa fadhili za Bwana, Nchi imejaa fadhili za Bwana, Nchi imejaa fadhili za Bwana. X2

1. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu, Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa, fadhili za Bwana.

2. Kwa neno lake Bwana Mbingu zilifanyika, na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake, hukusanya maji ya bahari, huviweka vilindi, katika ghala.

3. Heri Taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake, toka Mbinguni Bwana Mungu huchungulia, huwatazama na wanadamu wote pia. 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa