Ingia / Jisajili

Bwana Ni Nuru Yangu

Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari | Zaburi

Umepakiwa na: Richard Samson

Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 3 Mwaka A
- Katikati Dominika ya 2 ya Kwaresma Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Bwana ni nuru yangu na wokovu na wokovu wangu x2.

1. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?

Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?

2. Neno moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta,

Nikae nyumbani mwa Bwana, Siku zote za maisha yangu.

Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.

3. Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana, Katika nchi ya walio hai.

Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa