Mtunzi: Julius Anari
> Mfahamu Zaidi Julius Anari
> Tazama Nyimbo nyingine za Julius Anari
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Julius Anari
Umepakuliwa mara 575 | Umetazamwa mara 2,339
Download Nota Download MidiChorus: Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, (tena) ni ngome ya uzima wangu nimwogope nani? x2 Watesi wangu na adui zangu, walijikwaa tena wakanguka walipokuwa wakinikaribia. Na moyo wako usiwe na hofu, umtumaini Mwokozi Yesu Kristu Mwana wake Mungu.
1. Furaha yangu mimi, kukushirikisha wewe (Furaha yangu mimi kukushirikisha wewe), ujue kwamba Mungu yupo tena yupo kati yetu.
2. Bwana ni kinga yangu tena nimwogope nani, (Bwana ni kinga yangu tena nimwogope nani), Bwana ni ngome yangu mimi sasa sina chakuogopa.
3. Nimeamua mimi na maisha yangu yote (Nimeamua mimi na maisha yangu yote), nitakaa nyumbani mwake Mungu milele na milele.