Mtunzi: Julius Anari
> Mfahamu Zaidi Julius Anari
> Tazama Nyimbo nyingine za Julius Anari
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Julius Anari
Umepakuliwa mara 157 | Umetazamwa mara 971
Download Nota Download MidiEe Bwana uwe sitara na nuru maishani mwangu. Maana wewe ndiye kinga na njia yangu milele. Utanihifadhi na mateso utanizungusha nyimbo, utanizungusha nyimbo nyimbo nyimbo za wokovu. Nitakufindisha na kukuonyesha njia 'takayoenda, nitakushauri jicho langu likikutazama.
1. Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa, heri Bwana asiyemhesania upotovu ambaye rohoni mwake hamna hila.
2. Nalikujulisha dhambi yangu na sikuuficha upotovu, nami nitayakiri maasi yangu kwake Bwana, anisamehe upotovu wa dhambi yangu.
3. Mfurahieni Bwana shangilieni enyi wenye haki , pigeni vigelegele vya furaha kwa pamoja, ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.