Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 733 | Umetazamwa mara 2,740
Download Nota Download MidiBWANA TUMA WATENDA KAZI (F.B. KITUYI)
Kiitikio:
Bwana tuma watenda kazi shambani,
Ooh! kwani mavuno shambani ni mengi
(mengi) lakini watenda kazi ni wachache. x2
1. Nimtume nani, nimtume nani aende, akavune yote shambani?
(Bwana tuma watenda, watume watenda kazi shambani.) x2
2. Itikeni nyote Mungu awatume shambani, mavuno ni mengi ni mengi:
(Bwana tuma watenda, watume watenda kazi shambani.) x2
3. Nimeitika nitume niende shambani, nikavune yote mavuno:
(Bwana tuma watenda, watume watenda kazi shambani.) x2
4. Ewe Bwana Mungu ndiwe mwenye shamba, twaomba ukawachague wanao:
(Bwana tuma watenda, watume watenda kazi shambani.) x2