Maneno ya wimbo
NITAKAA NYUMBANI
Kiitikio:
Nami nitakaa nyumbani, nitakaa nyumbani, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. x2
1. Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu; (Katika malisho majani mabichi, hunilaza. x2)
2. Kando kando ya maji matulivu ananiongoza Bwana; (Katika njia haki ananiongoza, Bwana wangu. x2)
3. Nipitapo Katika mabonde ya uvuli was mauti; (Siwezi kuogopa mabaya maana, yupo nami. x2)
4. Gongo lako nayo fimbo yako vinanifariji Ee Bwana; (Umeniandalia maza machoni, pa watesi. x2)
5. Umepaka kichwa changu kweli mafuta umenipaka; (Kikombe kimejaa na kimefurika, wema wako. x2)
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu