Maneno ya wimbo
Nyoosha mkono wako Bwana unisaidie, maji yamefika shingoni, nimo kilindini nitazama Bwana, Dunia ni nzito Bwana ona yanielemea, mahangaiko kila kukicha, machozi yamekuwa faraja yangu: Hima bwana (njoo) unisaidie, hima Bwana unisaidie x2
1. Misiba nayo magonjwa yasiyokoma, moyo wangu wapondeka maumivu yasiyokoma kila kukicha, fanya hima Bwana unisaidie
2. Ugumu wa maisha kwangu ni kikwazo, marafiki hata ndugu, wanicheka na kunisema kila kukicha, fanya hima Bwana unisaidie.
3. Maadui wamenizingira pande zote, wanawinda roho yangu kwa bidii, ili wapate kuniangamiza, fanya hima Bwana unisaidie
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu