Ingia / Jisajili

Corona

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Valentine Ndege

Umepakuliwa mara 298 | Umetazamwa mara 1,252

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Mungu Mwenyezi twakuomba tujalie Amani duniani (pia) tuonyeshe huruma yako (kwani sasa) hofu imetanda kote duniani, Twatubu kwako dhambi zetu Mungu wetu mwingi wa huruma (Bwana) sikiliza kilio chetu (pande zote) vilio misiba imetawala; Mawimbi na dhoruba kali chombo chetu kinazama Bwana utuvushe salama, Matumaini ya safari Bwana yamefifia, Bwana njoo utuokoe 1. Hofu imetanda duniani kote watu wanawaza kunawa mikono kwa sabuni na sio kutubu dhambi, tena wanavaa barakoa na sio utakatifu, Corona imezua hofu, Mungu wetu tuhurumie utuvushe salama. 2. Hofu imetanda duniani kote, tunapambana na Corona usiku na mchana, nasi adui shetani, tunajifungia ndani ili kulinda afya zetu, Corona imeua wengi Mungu wetu tuhurumie njoo utuokoe. 3. Hofu imetanda duniani kote, tunaposhindana na watu na watu wenye nguvu, wakaao gizani, vita ya ulimwengu hatuwezi kupigana, Bikira Bikira Maria muombezi wa Taifa tuombee kwa Mungu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa