Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 693 | Umetazamwa mara 2,098
Download NotaKiitikio:
Hatimaye tabasamu limechanua pote, mwokozi wetu amefufuka x2
Mashairi:
1.Siku ya juma Mariamu na Magdalena, walikwenda kaburini mapema wakalikuta lile jiwe limeviringishwa Bwana hayumo, amefufuka....
2.Mara malaika wenye mavazi meupe wakatokea, wakawaambia msiogope Yesu mnaye mtafuta yu hai mzima kaburi li wazi Bwana hayumo, amefufuka....
3.a)Njoni mataifa tumwimbie Bwana aliyefufuka yu mzima mzima mzima.
b)Nyimbo za furaha tumuimbie ngoma, zeze na matari tumchezee kristu mfufuka.
Hitimisho:
(Ukimya na huzuni vilienea, Bwana Yesu aliposulibiwa msalabani, hofu kilio dunia nzima ilitetemeka, Yesu alipotufia msalabani) Sasa tuna tabasamu, kwa furaha Mwokozi wetu, amefufuka aiye: (chareko na Vifijo nderemo vigelegele vyapigwa) Sasa tuna tabasamu, kwa furaha Mwokozi wetu, amefufuka aiye: (minyonyoro ya kuzimu ameivunja vunja) Sasa tuna tabasamu, kwa furaha Mwokozi wetu, amefufuka aiye: (ametukomboa utumwani mwa shetani) Sasa tuna tabasamu, kwa furaha Mwokozi wetu, amefufuka aiye: