Ingia / Jisajili

Ee Baba Mikononi Mwako

Mtunzi: E. Kalluh
> Tazama Nyimbo nyingine za E. Kalluh

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 4,731 | Umetazamwa mara 9,651

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Nimekukimbilia we Bwana nisiaibike milele ee Baba mikononi mwako naiweka roho yangu

1. Umenikomboa ee Bwana Mungu wa kweli/ Ee Baba mikononi mwako naiweka roho yangu.

2. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu/ Naam hasa kwa jirani zangu.

3. Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu/ walioniona njiani walinikimbia.

4. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa/ Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.

5. Maana nimesikia masingizio ya wengi/ Hofu ziko pande zote.

6. Lakini mimi nakutumaini wewe Bwana/ Nimesema, wewe ndiwe Mungu wangu.

7. Nyakati zangu zimo mikononi mwako/ Uniponye na adui zangu,nao wanaonifuatia


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa