Ingia / Jisajili

Ee Bwana Fadhili Zako 2

Maneno ya wimbo

                     KIITIKIO

Ee Bwana fadhili zako zikae nasi, Ee Bwana fadhili zako zikae nasi,

zikae nasi kama vile, tulivyokungoja wewe.

                    MASHAIRI

  1. Mpigieni vigelegele enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
  2. Mshukuruni Bwana Mshukuruni Bwana kwa kinubi cha nyuzi kumi mwimbieni mwimbieni sifa.
  3. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili na kazi yake yote huitenda huitenda huitenda kwa uaminifu.
  4. Huzipenda haki na hukumu nchi imejaa fadhili fadhili fadhili za Bwana.
  5. Tazama jicho la Bwana li kwao wamchao, wazingojeao fadhili zake.
  6. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti na kuwahuisha wakati wa njaa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa