Ingia / Jisajili

Salamu Maria

Mtunzi: Wolford P. Pisa (WPP)
> Mfahamu Zaidi Wolford P. Pisa (WPP)
> Tazama Nyimbo nyingine za Wolford P. Pisa (WPP)

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Wolford Peter Pisa

Umepakuliwa mara 832 | Umetazamwa mara 3,889

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

SALAMU MARIA

Salamu mama Maria (mama) uliye mwombezi wetu kwa mwanao,

wewe ni mama wa Mungu (wewe) uliyekingiwa dhambi dhambi ya asili.

Ee mama (Ee mama) Maria, tunakuja kwako mama kimbilio letu,

Ee mama (Ee mama) Maria, ndiwe kimbilio letu sisi wakosefu

MASHAIRI

  1. Tunakuja kwako, tunalia mbele yako, Ee mama yetu Maria, mama yetu nyota ya bahari tuombee.
  2. Bikira Maria ulipalizwa mbinguni, upo na watakatifu, mbinguni, huko uliko nasi tufike.
  3. Ee mama Maria, umebarikiwa sana kuliko wanawake, wanawake wote, wewe ni mama mama wa Mungu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa