Ingia / Jisajili

Ee Bwana Uwe Pamoja Nami

Mtunzi: Felician Albert Nyundo
> Tazama Nyimbo nyingine za Felician Albert Nyundo

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Zaburi

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 7,125 | Umetazamwa mara 13,050

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Ee Bwana, uwe pamoja nami katika taabu zangu zote x 2
 
Mashairi:
 
1. Aketiye mahali pa siri pake aliye juu, atakaa katika uvuli wake Mwenyezi / 
Nitasema Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
 
2. Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitakaribia hema yako / 
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako zote.
 
3. Mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe / 
utawakanyaga simba na nyoka, mwana wa simba na joka utawaseta kwa miguu. 

Maoni - Toa Maoni

Toa Maoni yako hapa