Ingia / Jisajili

Ee Mungu Kwa Wema Wako

Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Richard Samson

Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 22 Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee Mungu Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa, uliwahifadhi walioonewa x2.

1. Wenye haki watafurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu; Naam, watapiga kelele kwa furaha. Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Furahini katika Bwana, shangilieni mbele zake.

2. Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani, Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa.

3. Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema, Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu. Kabila lako lilifanya kao lake huko; Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa