Ingia / Jisajili

Haya Ngoja Niimbe

Mtunzi: Erick Mwaniki
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Mwaniki

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 90 | Umetazamwa mara 565

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
HAYA NGOJA NIIMBE Nimeyasikia yale unayotenda, nimeona pia unayotenda kwangu maisha ni bure bila uwepo wako, hivyo basi kuwa nawe ni vyema, Moyo wangu una raha, raha tele, kwa yale yote Bwana utendayo Haya ngoja niimbe, wimbo mtamu, midundo ya kikwetu vinanda tunakuchezea, niache mimi niimbe, wimbo mtamu, sauti tamu tamu kayamba tunakuchezea. Umeniokomboa kwa msalaba wako, ukakufa kwa sababu ya dhambi zangu, huo ni upendo utokao kwa Baba, we’ unanipenda mi’ mtumishi wako. Kwa upendo ninaimba, sifa zako, mi’ nihubiri watu wakujue Ukanitetea ukasimama nami, wewe nuru yangu pia wokovu wangu, nakutegemea wewe unayeishi, unayetawala vyote vilivyo humu Mungu wa huruma tele, wastahili, kuheshimiwa pia kutukuzwa Jina lako litukuzwe lihimidiwe, neno lako litangazwe kwa mataifa, wakujue wewe na wakupende wewe, wakutumikie ndio ma’na naimba kwani niimbapo nyimbo, wasikika, unawaguza wageuza nyoyo.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa