Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO
Umepakuliwa mara 1,897 | Umetazamwa mara 4,811
Download Nota Download MidiKiitikio
Heri waendao katika sheria, sheria ya Bwana. x2
(Ee Bwana unifundishe amri zako, nami nitazitii siku zangu zote,
kwa moyo wangu wote.)x2
Mashairi
1.Heri walio kamili njia zao, waendao katika sheria ya Bwana, heri wazitiio shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wote.
2.Wewe umetuamuru mausia yako ili sisi tuyatii milele, ningependa njia zangu ziwe thabiti, nizitii amri zako zote.
3.Mtendee mtumishi wako ukarimu, nipate kuishi na kutii amri zako, ufumbue macho yangu niyatazame maajabu katika sheria yako.