Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Mwanzo
Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO
Umepakuliwa mara 1,986 | Umetazamwa mara 4,779
Download Nota Download MidiKiitikio
Wewe Bwana usiniache Mungu wangu, ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana wa wokovu wangu.x2
Shairi
1(a).Umekuwa msaada wangu, Bwana Mungu wangu, usinitupe.
(b).Nimejua na sheria zako, kamilifu sana, uniokoe.
2(a).Nimekuwa mdhaifu sana, tena mnyonge sana, unifadhili.
(b).Utazame na mateso yangu, nazo dhiki zangu, uniinue.
3(a).Upigane na adui zangu, wenye hila mbaya, niwe imara.
(b).Nimeacha njia zangu mbaya, na kukurejea, wewe mwenyewe.