Ingia / Jisajili

Ingawa Hakutenda Jeuri

Mtunzi: Gaudence F. Mtui
> Mfahamu Zaidi Gaudence F. Mtui
> Tazama Nyimbo nyingine za Gaudence F. Mtui

Makundi Nyimbo: Kwaresma

Umepakiwa na: Gaudence Mtui

Umepakuliwa mara 730 | Umetazamwa mara 2,530

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

HAKUTENDA JEURI

Ingawa hakutenda jeuri kinywani mwake hapakuwa na hila, lakini Bwana aliridhika kumchukua amemhuzunisha x2

  1. Kama mzizi katika nchi kavu, yeye hakuwa na umbo na uzuri, alitengwa na alidharauliwa, mtu aliyejaa huzuni nyingi.
  2. Amechukua masikitiko yetu, amejitwika pia huzuni yetu,tulimdhania amepigwa na Mungu, alijeruhiwa kwa makosa yetu.
  3. Alichubuliwa kwa maovu yetu kwa kupigwa kwake sisi tumepona,sote kama kondoo tumepotea, kila mmoja ameshika njia yake.
  4. Kwa kuonewa pia kuhukumiwa,aliondolewa aliondolewa,na maisha yake maisha yake, ni nani atakayeisimuliwa.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa