Mtunzi: Mwarabu Flowin Kaiza
> Mfahamu Zaidi Mwarabu Flowin Kaiza
> Tazama Nyimbo nyingine za Mwarabu Flowin Kaiza
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Flowin Mwarabu
Umepakuliwa mara 651 | Umetazamwa mara 2,111
Download Nota Download MidiKIITIKIO:
Ingia (bwana Yesu) ndani mwangu,
ingia (ndani bwana Yesu) itakase roho yangu.
Ingia (bwana Yesu) ndani mwangu,
ingia (ndani bwana Yesu) ishibishe roho yangu.
MAIMBILIZI:
1: Mwili wako ni chakula cha roho yangu
damu yako ni kinywaji cha roho yangu.
"ingia (Yesu) nipatie uzima"
2: Tazama naja kwako unipokee
nistahili kushiriki karamu yako
"ingia....."
3: Wewe ni bwana wangu na Mungu wangu
najongea nionje upendo wako
"ingia....."
4: Karibu bwana Yesu ndani mwangu
nami niweze kukaa ndani yako
"ingia......"
5: Unishibishe nisiwe na njaa tena
na uninyweshe nisiwe na kiu tena
"ingia....."