Mtunzi: Mwarabu Flowin Kaiza
> Mfahamu Zaidi Mwarabu Flowin Kaiza
> Tazama Nyimbo nyingine za Mwarabu Flowin Kaiza
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Flowin Mwarabu
Umepakuliwa mara 909 | Umetazamwa mara 3,016
Download NotaHiki ni kipindi cha Kwaresma muda wa kutubu
muda wa kujiandaa kufufuka na Yesu.
na tuitafakari kwa kina njia ya msalaba,
kukubali kuteseka pamoja naye Kristu.
na tujirudi tujitakase, kumrudia Mungu kwa machozi
sala, toba, kufunga na kujitoa kwetu...*2
MAIMBILIZI:
1. Kufunga ni kuamua kujitesa
kujinyima tuvipendavyo kwaajili ya wenzetu,
hasa wenye shida.
2. Sala zisiwe ni za maonyesho
uingie sirini mwako bwana atakuona,
na atakujibu.
3. Toba iwe ya kutoka moyoni
kusudia kuacha dhambi na kujitenga nazo,
na kuziungama.