Ingia / Jisajili

Sifa Zivume

Mtunzi: Mwarabu Flowin Kaiza
> Mfahamu Zaidi Mwarabu Flowin Kaiza
> Tazama Nyimbo nyingine za Mwarabu Flowin Kaiza

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Flowin Mwarabu

Umepakuliwa mara 1,248 | Umetazamwa mara 3,269

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO:

    Sifa zivume kwake Mungu wetu, matendo yake ni ya ajabu, asifiwe.

            njoni tuimbe pia na tucheze, na tufanye shangwe kwa jina lake asifiwe.

maimbilizi:

       1: Yeye aliumba ulimwengu na vilivyomo mimea, wanyama viumbe vyote.

       2: Alifanya njia baharini, maji ya sham, wanaisraeli wakayavuka.

       3: Bwana aliwanyeshea mana waisraeli wakala jangwani

KIBWAGIZO CHA KUMALIZIA:

       Yote aliyoyatenda bwana hatuyastahili, ni neema zake hivyo;

                  basi tuyakumbuke matendo yake makuu,

                   basi tukumbuke mema yasiyohesabika

                    hivyo tuungane na tuimbe sifa zake

                    ngoma na makofi vifijo na vigelegele

                        asifiwe.......ASIFIWE!!!!


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa