Ingia / Jisajili

KIINI CHA NGANO.

Mtunzi: Gabriel Kapungu
> Mfahamu Zaidi Gabriel Kapungu
> Tazama Nyimbo nyingine za Gabriel Kapungu

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Gabriel Kapungu

Umepakuliwa mara 298 | Umetazamwa mara 1,750

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIINI CHA NGANO:

Kiini cha Ngano Tunda la mzabibu. x2. Bwana Yesu katenda maajabu maajabu ya kweli, Mataifa yainua mikono huyu mwana wa Mungu. Kwa mikate mitano na Samaki watu wengi washiba, Pale Kana Harusi imefana  Maji yawa Divai, (twende) twende tumpokee, (twende) twende tumpokee. X2.

1: Tujongee Meza yake twende tumpokee, tena twende kwa furaha twende tumpokee. Bwana yesu kajitoa Sadaka , Mwili wake pia na Damu yake. Twende tumpokee.

2: Mimi wewe yule wote twende tumpokee, wanaume kwa wanawake twende tumpokee. Tunyenyekee mbele zake Mungu, kwa magoti na kusali kwa Moyo. Twende tumpokee.

3: Tuchunguze nafsi yetu twende tumpokee, tukijihoji wenyewe twende tumpokee. Twastahili kula mwili wa Bwana, na kukila Kikombe cha baraka. Twende tumpokee.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa