Ingia / Jisajili

Maagizo Ya Bwana

Mtunzi: Erick Mwaniki
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Mwaniki

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani | Zaburi

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 149 | Umetazamwa mara 546

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Maagizo ya Bwana ni adili, huufurahisha moyo, huufurahisha moyo, maagizo ya Bwana ni adili, huufurahisha moyo*2 1. Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi, huiburudisha nafsi Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia, humtia mjinga hekima. 2. Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele, kinadumu milele Hukumu za Bwana ni kweli, ni kweli Zina haki kabisa, zina haki kabisa 3. Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri, mambo ya siri. 4. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi, yasinitawale mimi Ndipo nitakapokuwa kamili, nitakapokuwa kamili Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa