Ingia / Jisajili

MAANA KWA BWANA KUNA FADHILI NA KWAKE KUNA UKOMBOZI MWINGI

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 716 | Umetazamwa mara 1,829

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Maana kwa Bwana kuna fadhili, na kwake kuna ukombozi, na kwake kuna ukombozi ukombozi mwingi. 1.Ee Bwana toka vilindini nimekulilia, Bwana uisikie sauti yangu, masikio yako na yasikilize sauti ya dua zangu. 2.Bwana kama wewe ungeyahesabu maovu, ee Bwana kweli nani angesimama, lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe. 3.Nimemngoja Bwana na roho yangu imengoja, na neno lake nimelitumainia, nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi waingojavyo asubuhi. 4.Ee Israeli umtarajie Bwana, maana kwa Bwana kuna fadhili na kwake kuna ukombozi mwingi, atamkomboa Israeli na maovu yake.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa