Ingia / Jisajili

MATAIFA YOTE YA ULIMWENGU WATAKUSUJUDIA EE BWANA

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Epifania | Noeli | Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 650 | Umetazamwa mara 2,410

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Mataifa yote ya Ulimwengu, mataifa yote ya ulimwengu watakusujudia wewe, watakusujudia wewe, watakusujudia wewe ee Bwana. 1.Ee Mungu mpe mfalme hukumu zako, na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, na watu wako walioonewa kwa hukumu. 2.Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hata bahari, toka mto hata miisho ya dunia. 3.Wafalme wa tarshishi na visiwa na walete kodi, wafalme wa sheba na seba na watoe vipawa. Naam wafalme wote na wamsujudie, na mataifa yote wamtumikie. 4.Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo, na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, na nafsi za waitaji ataziokoa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa