Maneno ya wimbo
Mungu mpangaji
Eric Mwaniki FRANCIS, SJ
1. Binadamu anapanga mambo mengi atakayofanya siku zijazo,
anawaza vyema na tena anatumia uzoefu alionao,
atumaini, yote yatatimia
anaamini, yupo Mungu muweza
Ni Mungu muumbaji wa mbingu na dunia aliyeweka vitu vyote pale vistahilivyo
Mungu mpangaji wa mambo yaishiyo na mambo ya milele tumaini la mwanadamu
2. Jumatatu hadi jumamosi anajishungulisha na utafutaji,
kisha siku ya saba anaamka na kuelekea madhabahuni,
kumshukuru, yeye aliye juu,
na kumsifu, yeye Mungu muweza
3. Anajishungulisha na familia yake kuwalea watoto wake
wala hajishungulishi na mambo yanayoshinda ule uwezo wake
ye' anajua, Mungu ampigania
ye' ameweka, tumaini kwa Bwana
4. Anajitenga na mabaya na dhambi kwani zina mkwaza Mungu wake,
katika mambo mengi duniani anatamani moja tu litimie
anatamani, ampendeze Mungu
ili mwishoni, amlaki nyumbani
5. Hata kwa magumu hafi moyo anamlilia Mungu mwenye uwezo,
anajua kuwa hataaibika akimuita atamsikia
atamjibu, kumfuta machozi
nakumtia, nguvu na neema zake
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu