Mtunzi: Sebastian Don Ndibalema
> Mfahamu Zaidi Sebastian Don Ndibalema
> Tazama Nyimbo nyingine za Sebastian Don Ndibalema
Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma | Matawi
Umepakiwa na: Sebastian Ndibalema
Umepakuliwa mara 840 | Umetazamwa mara 2,457
Download Nota Download MidiMungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha, Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha x 2
1. Wote wanionao hunicheka sana, hunifyonya wakitikisa vichwa vyao/
Husema: Umtegemee Bwana na amponye, na amwokoe sasa maana apendezwa naye
2. Kwa maana mbwa wamenizunguka, kusanyiko la walevi wamenisonga/
Yamenizua mikono na miguu, naweza kuihesabu mifupa yangu yote
3. Wanagawana nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura/
Nawe Bwana usiwe mbali, Ee Mungu wangu fanya haraka kunisaidia
4. Nitalihubiri Jina lako kwa ndugu zangu, katikati ya kusanyiko nitakusifu/
Ninyi mnaomcha Bwana msifuni, Enyi wote mlio mzao wa Yakobo mtukuzeni