Maneno ya wimbo
MWIMBIENI BWANA ZABURI
Mwimbieni Bwana zaburi watauwa wake Mwimbieni Bwana Na kufanya shukrani
(kwa maana) Kwa kumbukumbu la utakatifu wake, nitamtukuza maana ameniinua, *2
Mwimbieni Bwana zaburi watauwa wake Mwimbieni Bwana Na kufanya shukrani
1. Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu (Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia (kulilia) Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya.) *2
2. Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu, kutoka kuzima, Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.
3. Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.
Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. (Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.)*2
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu