Ingia / Jisajili

Salamu Mama Maria

Mtunzi: Erick Mwaniki
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Mwaniki

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Mama Maria | Shukrani

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 122 | Umetazamwa mara 651

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
SALAMU MAMA MARIA Salamu mama yetu Maria *2 Mama uliyekingiwa Dhambi ya asili, msaada wa wakristo mlango wa mbinguni, (saalam Maria, Maria saalam) *2 1. Tazama dunia hii machafuko mengi, amani upendo, vyote vimetoweka, tunakulilia ee mama mwema mama tuombee 2. Familia zetu hizi zasambaratika, upendo haupo, tena vita ni vingi, tunakulilia ee mama mwema mama tuombee 3. Tazama vijana wetu ndio tegemeo, ila waangamia madawa ya kulenya, tunakulilia ee mama mwema mama tuombee 4. Tazama Watoto wetu hawana malezi, wengi mayatima wako barabarani, tunakulilia ee mama mwema mama tuombee 5. Tazama Maisha yetu tunahangaika, furaha haimo shida ni nyingi sana, tunakulilia ee mama mwema mama tuombee

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa