Mtunzi: Traditional
> Tazama Nyimbo nyingine za Traditional
Makundi Nyimbo: Juma Kuu
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 3,284 | Umetazamwa mara 8,414
Download Nota Download Midi1.Nakuakuabudu Mungu wangu ujifichaye altareni,ninakutolea moyo wangu usiofahamu siri yako (Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu milele, milele milele u mtakatifu, utukuzwe milele yote katika Hostia Takatifu
2.Mafahamu yangu yadanganya yakwunapo pia kugusa, nami ninakupa moyo wangu usiofahamu siri yako (Mtakatifu..........)
3.Wauficha u-Mungu wako msalabani na ubinadamu wako altareni, nami naungama yote mbili kama mwivi yule mwenye toba (Mtakatifu.....)
4.Thomaso aligusa majeraha nami nasadiki bila shaka,Ee Yesu nipe pendo lako nikwamini wewe kwa imani. (Mtakatifu......)
5.Umeteswa nini bwana mwema kwa kunipa mkate wa uzima, Yesu unifiche ndani yako ili nionje pendo lako(Mtakatifu.....)
6.Yesu pelicane utazame na kwa damu yako nitakase, tone moja ndilo lanitosha na dunia yote yaokoka (Mtakatifu....)
7.Ndani ya mafumbo Yesu yumo utafunguliwa kwangu lini,nikuone Yesu uso wako nishiriki nawe heri yako (Mtakatifu.....)