Ingia / Jisajili

Sala Ya Kuwaombea Mapadre

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Juma Kuu | Kristu Mfalme | Mafundisho / Tafakari | Miito

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 878 | Umetazamwa mara 3,009

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

SALA YA KUWAOMBEA MAPADRE

  1. Ewe Ye-su kasisi Mkuu na Mpakwa mafuta wa- Mungu, upokee sala ye-tu kuwaombea makasisi we-tu. Uwalinde na mabaya yo-te wafariji katika upwe-ke, Ibariki-ki mikono yao inayotubariki si-si.
  2. Ewe Roho Mtakatifu ndiwe tunda la uadilifu, Kiongozi wa kiroho na zawadi ya mwokozi wetu. Wajalie tunu ya usafi, uwakinge na adui mbaya, wahifadhi kwenye moyo wa Yesu wasichafuke roho zao.
  3. Kwa unyenyekevu mkuu tunaomba kwako Bwana mwema, kwa uwezo wa pekee na umungu wako wa ajabu! katika upweke wafariji, waongoze hata kwenye hofu, wajalie watambue kwamba katika mateso roho zasafishwa
  4. Hata sisi wana wako, tusiostahili mbele zako. tujalie kuwapenda na kuwatunza makasisi wetu. Tusiwakatishe tamaa wanapofanya kazi yako, kwani kwa njia ya mapadre tunapata wokovu
  5. Ee Maria Mtakatifu, ndiwe mama wa mapadre wetu. Yesu alikukabidhi alipokuwa msalabani. Waombee tunu ya utii, ubikira na umasikini, waongoze ili watuongoze, kwenye makao ya milele. AMINA


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa