Ingia / Jisajili

Mtetezi Wangu Yu Hai No 2

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 943 | Umetazamwa mara 5,762

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

MTETEZI WANGU YU HAI ( Ayubu 19:25; Warumi 8: 18, 29-30, 35-39)

Najua kwa hakika, mtetezi wangu yu hai, nayakuwa baada ya yote mimi nitashinda. x2 Kitu gani kitanitenga na Mungu anayenipenda, ninakaza mwendo nifikie taji takati-fu la ushindi.x2

1. Hakika najua Mungu ninayemtumikia, hawezi kuniacha ni-shindwe na dunia, huruma yake itanifunika ili nisianguke milele

2. Kwa maana nayahesabu mateso ya sasa kuwa si kitu kama ule utukufu utakaofunuliwa kwetu

3. Basi tuseme nini sasa juu ya hayo, Mungu akiwa upande wetu nani aliye juu yetu

4. Ma ana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua wafananishwe na mfano wa mwanaye. Hao akawaita na kuwahesabia haki, akawaweka miongoni mwa watakatifu wake.


Maoni - Toa Maoni

filemon pius Jan 17, 2018
mpovizur mungu awepamoja na nyie

Toa Maoni yako hapa