Ingia / Jisajili

Salaam Maria

Mtunzi: Dr. Nicholas Azza
> Mfahamu Zaidi Dr. Nicholas Azza
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Nicholas Azza

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Nicholas Azza

Umepakuliwa mara 161 | Umetazamwa mara 580

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
SALAAM MARIA 1. Salaam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe Maria. Umebarikiwa kuliko wanawake, wanawake wote duniani. Naye Yesu, Bwana wetu, mzawa wa tumbo lako, amebarikiwa sana. Ewe Maria kwa utiifu wako umeleta wokovu duniani. Mama Maria utufundishe kuwa watiifu kwa maagizo ya Mungu. 2. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, Mama wa Kanisa. Utuombee sisi wakosefu, saasa na saa ya kufa kwetu. Ewe Mama wa Rehema, Ewe Bikira Msafi, uwe shauri na kimbilio letu. Ewe Maria, moyo wako ulichomwa na kifo cha mwanao. Sasa Maria tusaidie kuvumilia mateso yetu. Amina.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa