Mtunzi: Patrick Wambua
> Mfahamu Zaidi Patrick Wambua
> Tazama Nyimbo nyingine za Patrick Wambua
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: patrick wambua
Umepakuliwa mara 431 | Umetazamwa mara 1,580
Download Nota Download MidiSop: Tusimame sote twende kwa Bwana,
All: Na zawadi zetu, tukampe Bwana,
Sop/Alto: Peleka vipaji vyote kwa Bwana,
All. Na Bwana Mungu wetu atapokea x2
1. Mkate ni zao, ni zao la shamba, ni kazi ya mikono yetu twaomba pokea.
2. Divai ni tunda, tunda la mzabibu, ni kazi ya mikono yetu twaomba pokea.
3. Fedha za mifuko, ni juhudi yetu, bidii ya mikono yetu twaomba pokea.
4. Twaleta nafaka, kutoka shambani, tunakusihi kwa huruma twaomba pokea.
5. Nafsi zetu pia, twazileta kwako, na sala zetu pia Baba twaomba pokea.