Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Moyo Mtakatifu wa Yesu | Ndoa
Umepakiwa na: Stanslaus Butungo
Umepakuliwa mara 2,720 | Umetazamwa mara 7,754
Download Nota Download Midi(1Kor 13: 1,3-7; Yohana 13:15; Mathayo5:44-48, 7:7)
Nijaposema kwa lugha za wanadamu, nijaposema kwa lugha za malaika, kama mimi sina upendo sifai kitu kamwe. Tena nikiutoa mwili wangu uungue moto kama sina upendo sifai kitu kabisa. Nami najua ya kuwa kwamba hakuna upendo mku-bwa kama kutoa uhai wa-ngu, kwa ajili ya rafiki marafiki zangu, tena nimejifunza kwa Kristu; Mungu kuuacha umungu wake na kutwaa ubinadamu, kushiriki ubinadamu wetu na kufa msalabani, (upendo wa ajabu sana upendo wa kweli) x2
Tazama ninaposhi-ndwa kumsamehe ndugu yangu anaponikosea ninaonesha mfano gani kwa watu, maana hata wenye dhambi hushindwa kusamehe. Ukristu wangu ni nini kama nakuwa mbinafsi na kushindwa kabisa kujali maumivu na shida za watu, natofautiana nini na wasio wa kristu? Nimpende jirani yangu kama ninavyojipenda mimi, nikubali kuitesa nafsi yangu kwa ajili ya furaha yake, na huo ndio ufuasi wa kweli wa Kristu.
Upendo huvumilia, upendo hautakabali,hautafuti mambo yake, haufurahii udhalimu, upendo ni unyenyekevu, daima kukishinda kiburi, ni kutokuhesabu mabaya, wanayotutendea wengine. Yanadumu mambo matatu, Imani matumaini, mapendo, lakini sote twajua, tunajua lililokuu ni UPENDO x 2