Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Norbert Hamaro
Umepakuliwa mara 13 | Umetazamwa mara 18
Download Nota Download MidiAlimwalika Petro kutembea juu ya maji mengi nayeye akatembea hatua kadhaa (Petro) njiani akaogopa mawimbi yakamyumbisha (Petro) na Yesu akamwambia usiogope kabisa (Amini) Imani ndiyo silaha ukimwamini mwokozi (Yesu) yawe maji yawe mawimbi hakika utavuka salama tu..!
Usiogope Kabisa nenda Bwana Yesu atakulinda tu mtazame kwa imani nenda Bwana Yesu atakulinda tu (Mawimbi yakijaa nenda Bwana Yesu atakulinda tu Bwana Yesu ni Mwaminifu ukimuamini nenda×2)
1. Duniani kuna shida taabu mahangaiko yanatanda mbele yetu kututisha tusipite tukiyaogopa hayo hatutatenda lolote tutabaki lialia tutapoteza yoote. Yesu anatualika tumtazame daima tuyakanyage maji yote tusonge mbele (tutafika tu..!)
2. Mbingu siyo lele mama hatufiki kirahisi sadaka na msalaba mateso ndiyo mapito ibada na kujinyima kwa ajili ya wengine kuukataa uhuru kuwa watumwa wa Mungu. Yesu anatualika tujikane nafsi zetu tubebe misalaba yetu tusonge mbele (tutafika tu..!)
3. Tusitazame pembeni tusiyatazame mawimbi yatatujengea hofu yatayumbisha imani macho yatazame mbele alipo Yesu mwokozi fadhili za Bwana Mungu zi mbele yetu daima. Yesu anatualika tuamini anaweza tukanyage bila mashaka tusonge mbele (tutafika tu..!)