Ingia / Jisajili

Waipeleka Roho Yako

Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho

Makundi Nyimbo: Pentekoste

Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO

Umepakuliwa mara 862 | Umetazamwa mara 2,597

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Pentekoste

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

Waipeleka Roho yako Ee Bwana (nawe) waufanya upya uso wa nchi.x2

Mashairi

1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana, wewe ni Bwana tena ni Mungu wangu, umejifanya mkuu sana umejivika heshima na adhama.

2.Jinsi yalivyo mengi matendo yako, na kwa hekima umevifanya vyote, dunia imejaa mali zako uhimidiwe Ee Mungu wa milele.

3.Waiondoa pumzi yao Bwana, nao wakifa hurudi mavumbini, waipeleka Roho wanaumbwa nawe waufanya upya uso wa nchi.

4.Na Utukufu wake Bwana udumu, Bwana afurahie matendo yake, kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake nami nimfurahie.


Maoni - Toa Maoni

William alleni msangi Mar 12, 2017
Kwakweli mungu akubariki utengeneze kigongo kingine kiweze kudumu kamakilivyo dumu hiki am in a barikiwa sanaaa.

William alleni msangi Mar 12, 2017
Kwakweli mungu akubariki utengeneze kigongo kingine kiweze kudumu kamakilivyo dumu hiki am in a barikiwa sanaaa.

Toa Maoni yako hapa